Archive for March, 2011

Spika kutoka chama cha MDC ashinda tena Zimbabwe

Posted in Uncategorized on March 30, 2011 by sunday Shomari


Hali ya wasiwasi ilitanda katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare Jumanne, huku chama cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai Movement For Democratic Party kikishinda kile cha Bw. Mugabe ZANU-PF katika uchaguzi wa spika wa bunge.

Kwa mujibu wa VOA uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku baadhi ya wabunge wakiwa wamefungwa jela wakati wa kura hiyo.

Spika wa zamani Lovemore Moyo anayefahamika kwa uungaji mkono wake kwa chama cha Bw. Tsvangirai alishinda tena kiti hicho, kura hiyo ikiashiria kuwa baadhi ya wabunge kutoka chama cha Bw. Mugabe walimpigia kura.

Chama hicho cha MDC kilishinda kile cha ZANU-PF katika uchaguzi wa wabunge mwaka wa 2008.
Uchaguzi wa Jumanne wa spika la bunge ulifuatia maamuzi ya mahakama kuu ya Zimbabwe kuwa kuchaguliwa kwa Bw. Moyo katika uchaguzi wa kwanza mwaka wa 2009 hakukuwa halali, na hivyo ikabidi uchaguzi wa kiti hicho ufanyike tena.

Na ingawa dazeni za wabunge kutoka vyama vyote vitatu wameaga dunia tangu mwaka wa 2008, makubaliano ya kisiasa katika serikali ya Umoja wa Kitaifa yanapiga marufuku uchaguzi mdogo.
ZANU-PF ilimteuwa mwenyekiti wa chama Simon Khaya kugombania kiti cha Spika, huku Bw. Tsvangirai akiamua kumteuwa tena Lovemore Moyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake.

Chama kidogo kilichojitenga na chama cha MDC kinachoongozwa na Welshman Ncube hakikumteuwa mgombea na kilikuwa kimeahidi kuwa wabunge wake hawatashiriki katika kura hiyo. Lakini Jumatatu chama hicho cha Ncube kiliamua kumuunga mnkono Lovemore Moyo kikisema kuwa kukamatwa kwa wabunge wa chama cha Bw. Tsvangirai umehujumu demokrasia.

Mbunge wa ngazi ya juu wa chama cha MDC ambaye bado yuko gerezani ni waziri wa nishati Elton Mangoma aliyekamatwa Ijumaa iliyopita. Mangoma ana ulemavu wa miguu na huchechemea anapotembea.
Hata hivyo kulikuwa na shamra shamra baada ya chama cha upinzani MDC kushinda kiti hicho cha spika wa bunge la Zimbabwe.

Sumaye yuko huru kuanzisha chama chake -UVCCM.

Posted in Uncategorized on March 29, 2011 by sunday Shomari


Waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye.
Chama cha Vijana wa CCM (UVCCM) kupitia katibu mkuu wake Martin Shigela hivi karibuni kimetoa maelezo ya kumshauri waziri mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa anachofanya kile alichokiita uhuru wa kutoa maoni yake ni utaratibu tofauti na wao na wanamkumbusha kuwa tabia yake haiwezi kuvumilika na anao uhuru wa kuanzisha chama chake kama angependa. Kulikoni?
Sikiliza taarifa kamili kwa mujibu wa mwandishi wa Sauti ya Amerika (VOA) Daressalaam Dina Chahali. Bofya hapa chini.


<img

Hotuba ya Obama juu ya Libya

Posted in Uncategorized on March 29, 2011 by sunday Shomari


Rais wa Marekani Barak Obama amesema nchi yake ilijiunga katika kampeni za kijeshi za mataifa ya magharibi dhidi ya kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi, kuzuia mauaji na kumaliza utawala unaokandamiza watu wa Libya.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA)katika hotuba yake kwa taifa iliyotangazwa kwenye televisheni, amesema kuwa kampeni hizo zilizohalalishwa na Umoja wa Mataifa zimezuia mauaji ya raia kutoka kwa kiongozi huyo wa Libya.

Rais amesema kuwa Bw. Gadhafi amepoteza imani kwa watu wake na haki ya kuongoza, na kuongeza kuwa “hakuna shaka kuwa Libya, na dunia kwa ujumla, itakuwa salama zaidi “ ikiwa Bw. Gadhafi hatokuwa madarakani.

Lakini akasema kuwa kupanua harakati za kijeshi na kujumuisha mabadiliko ya utawala nchini Libya litakuwa ni kosa.

Bw. Obama pia alizungumzia umuhimu wa kumzuia Bw. Gadhafi kuwaadhibu wale wanaompinga, jambo ambalo linaweza kusababisha kile ambacho kingeonekana kama mgogoro wa kibinadamu.

Akizungumza na sauti ya Amerika, mara baada ya hotuba hiyo, Prof. Ladi Madosh Makene wa Chuo kikuu cha Clark mjini Boston alisema rais Obama ametetea vyema maamuzi ya utawala wake na kujaribu kutuliza wakosoaji wake juu ya hatua aliyochukua ya kijeshi dhidi ya Moammar Ghadafi.

Dinner muhimu na Mzee Shirima.

Posted in Uncategorized on March 28, 2011 by sunday Shomari


Mzee Shirima akitoa ukaribisho maalum.

Nikiwa na Stella Shirima na kulia Bi.Lulu

Kutoka kushoto Mama Shirima, Richard, Stella na wajukuu wa Mzee Shirima.

Nikipata wasaa wa kung’aa na Mzee Shirima.

Mama Shirima na Jen Mushumbusi.
Kwa picha zaidi bofya Read more »

Babu Kaju atoa kibao na mkongwe Carlos Santana

Posted in Uncategorized on March 28, 2011 by sunday Shomari


Mkongwe Carlos Santana.

Babu Kaju.
Alex Kajumulo a.k.a Babu Kaju amekuwa katika katika harakati zake za kukuza muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania kwa kushirikiana na wakongwe mbali mbali hayati Cool James, Mbilia Bel,baadhi ya wakongwe wa The Wailers na wengineo sasa mwanamuziki huyu ameshirikiana na mkongwe Carlos Santana kwenye kibao “Like Me” bonyeza hapa chini usikilize kibao hicho kinavyorindima.


Waasi Libya watwaa miji zaidi

Posted in Uncategorized on March 28, 2011 by sunday Shomari


Waasi wa Libya wameitwaa tena miji kadhaa ya ufukweni inayokaribiana na Sirte, baada ya mashambulizi ya makombora kutoka ndege za majeshi ya muungano wa NATO .

Kwa mujibu Sauti ya Amerika (VOA) Edward Yeranian anaripoti kuwa majeshi ya waasi wa Libya yamefanikiwa kusonga mbele kwa haraka, wakichukua tena bandari muhimu za miji ya mafuta za Ras Lanouf na Brega, ambazo zilitwaliwa na majeshi ya serikali takribani siku kumi zilizopita.

Mashahidi wanasema majeshi ya serikali yalijitoa katika eneo hilo bila mapigano yoyote. Baadhi ya wanajeshi waliobaki eneo hilo walijisalimisha.

Televisheni ya Al-Arabia Jumapili ilionyesha picha za vifaru vya serikali vilivyoteketezwa pamoja na magari ya kijeshi katika barabara kuu ya pwani inayoelekea mji wa Ras Lanouf. Pia ilionyesha video ya ndege za Uingereza zikilipua maeneo kadhaa yanayokaliwa na Gadhafi.

Wanajeshi waasi wameiambia Televisheni ya Al-Jazeera kwamba harakati zao zijazo zitaelekezwa mji wa bandari ya Sirte, mji anaotoka kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi. Kanali wa zamani wa jeshi ambaye amejiunga na waasi amesema kuwa majeshi yanayomtii Gadhafi yametega mabomu ya ardhini kuzunguka mji wa Sirte.

Mambo yalivyokuwa Kili Music Awards Diamond Jubilee

Posted in Uncategorized on March 27, 2011 by sunday Shomari


Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Mama Juhayna Kusaga akimpa tuzo mtayarishaji man water kwa niaba ya mwanamuziki 20% aliyejizolea tuzo 5 ikiwa ni pamoja na mwimbaji bora wa kiume, wimbo bora wa Afro Pop, wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa nyimbo na msanii bora wa muziki wa kiume.

Msanii maarufu wa Ze Comedy Mpoki akipokea tuzo ya msanii bora wa asili.


Msanii C-pwaa akipokea tuzo ya video bora ya muziki ya mwaka na wimbo wake ACTION ambao alishirikiana na Miss Trinity.

Wananchi waliofurika Diamond Jubilee wakisimama kwa dakika moja kuomboleza wasani wenzao wa Taarab waliopoteza maisha.

Msanii Lina akifanya vitu vyake.

Msanii mkongwe Lady Jay Dee ambaye sasa anatamba na kiota chake kipya cha maraha Sebuleni akiwa pia ni mjasiriamali amechukua tuzo mbioli msanii bora wa kike na wimbo bora Afrika Mashariki.

Hatimaye Mzee Mabella apata anachostahili kwa kupewa tuzo ya msanii binafsi (Hall of fame ).

Kushoto Mwanablog maarufu Othman Michuzi akiwa na mtalaam Soggy Lumanyika kwenye tuzo hizo.(Picha kwa hisani ya Othmani Michuzi-mtaa kwa mtaa blog).

Mgombea mwenza urais wa kwanza wa kike Marekani afariki.

Posted in Uncategorized on March 26, 2011 by sunday Shomari


Mgombea urais wa kwanza wa kike Marekani Geraldine Feraro.
Mama Geraldine Feraro mgombea mwenza urai wa kwanza wa kike hapa Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75 kwa ugonjwa wa kansa ya damu.

Mama huyu ambaye ndie amefungua njia kwa Hillary Clinton na Sara Palin kuwa na nafasi kubwa kwa wanwake hapa Marekani alipata nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa Walter Mandale mwaka 1984 alipogombea kiti cha urai dhidi ya Ronald Reagan na mgombea mwenza wake George Bush mkubwa.

Atakumbukwa sana katika medani za siasa hapa Marekani hasa na wakati huo alikuwa mbunge wa New York , katika salaam zake za rambi rambi Rais Obama amemwita kuwa ni mchapa kazi na atakumbukwa kwa kutetea haki za wanawake na haki kwa wote.

Syria nako kwawaka

Posted in Uncategorized on March 26, 2011 by sunday Shomari


Yale mambo ambayo tulifikiri hayawezekani kumbe bado yawezekana hivi karibuni lile wimbi la Mapinduzi katika nchi za kiarabu ndio sasa limekuwa kama tui la nazi kwenye mboga, kwani hivi sasa yaripotiwa huko Syria waandamanaji wanaodai uhuru wamekusanyika kote nchini humo Ijumaa ikiwemo mji mkuu Damascus na mji wa kusini ambapo katika mji wa Daraa karibu na mpaka na Jordan mamia ya watu walitembea kwa kile waandaaji walichokiita “ siku ya utu’ .

Vyombo vya habari vinasema hakukuwa na ulinzi ulioonekana katika mitaa ambako takriban watu 15 walikufa katika maandamano ya wiki hii.

Takriban watu 200 wengine waliandamana mjini Damascus baada ya sala ya ijumaa kuwaunga mkono watu wa Daraa.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kukamatwa kwa dazeni ya watu. Serikali ya Syria ilisema alhamisi itafikiria kuondoa sheria ya hali ya dharura nchini kama sehemu ya mlolongo wa mageuzi.

Alex Kajumulo atoa wimbo ulioshika namba 1 Jamaica na waimbaji wa Bob.

Posted in Uncategorized on March 26, 2011 by sunday Shomari


Alex Kajumulo a.k.a Babu Kaju.

Mwanamuziki ambaye anajulikana zaidi kama mpenda soka Alex Kajumulo “The Bushman” ametoa kibao akishirikiana na wanamuziki wa zamani wa Bob Marley kiitwacho It’s me Again Jah. Kajumulo aliyezungumza na Blog hii ameeleza kuwa wimbo huu sasa unakamata nambari moja hukokatika kisiwa cha Jamaica.

Kwa hiyo anesema ameweka historia ya kuwa mwanamuziki wa nje ya Jamaica kuweza kuwa na kibao nambari moja kwenye Radio Station za Jamaica , katika wimbo huu Kajumulo a.k.a Babu Kaju ameshirikiana na mwimbaji Selasie I Soldier na katika Bass ameshirikiana na mpiga Bass wa Bob Marley Clinton Fearon a.k.a Boogie Brown na mpiga Drums pia aliyewahi kuimba na Bob Marley halikadhalika Bob Carlton Barrett na unaweza kusikiliza kibao hicho kwa kubofya kitufe hapa chini.


Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,707 other followers