Archive for February, 2011
Rais Kabila anusurika shambulizi
Posted in Uncategorized on February 28, 2011 by sunday Shomari
Afisa mmoja wa serikali ya Congo anasema watu wenye silaha walivamia nyumba ya rais Joseph Kabila jumapili na kusababisha mapigano yaliouwa watu 7.
Bw. Kabila aliripotiwa kuwa yu salama na hajajeruhiwa na shambulio hilo ambalo lililenga nyumba yake katika eneo la Gombe katika mji mkuu Kinshasa.
Katika mahojiano na VOA msemaji wa serikali Lambert Mende alisema kiasi cha wapiginaji 50 walishambulia nyumba ya rais. Alisema walikuwa na silaha kali na nyepesi na mapanga.
Boston Celtics yapoteza wanne, Hasheem njia moja Houston.
Posted in Uncategorized on February 26, 2011 by sunday Shomari
Washabiki wa Boston ama kwa hakika watamkosa Perkins mwenye maguvu ya Nyati.

Bandari ya Boston inamuaga pia Nate Robinson.

Hasheem Thabeet kuingia Houston.
Katika hatua isiyotegemewa kwenye msimu huu wa kumaliza mabadilishano ya wachezaji kwenye Ligi maarufu ya kikapu NBA, timu kongwe ya Boston Celtics imetoa wachezaji wake wanne Kendrick Perkins,Nate Robinson ambao wanakwenda Oklahoma City Thunder na wao kumchukua mchezaji wa mbele Jeff Green na wa kati Nenad Krstic, wakati huo huo wachezaji wao chipukizi Semith Erden na Luke Haragody wanakwenda Cleveland Cavaliers.
Wachambuzi wa Basket ball wanajiuliza ni faida gani Boston wanaipata kumchukua Jeff Green amabaye ameonyesha mchezo hafifu sana mpaka sasa na kwa nini wamwache mchezaji mzuri na mwenye Mbwembwe kama Nate na mchezaji mwenye nguvu za nyati Kendrick Perkins? ama kwa hakika kwa mtaji huo Oklahoma City Thunder wana kicheko cha mwisho.
Mchezaji Kevin Garnet a.k.a KG alipohojiwa na waandishi wa habari aleleza kuumia kwake na roho kupoteza washirika wake wawili waliokuwa wakiisaidia sana timu hiyo na hasa ukizingatia wana mtihani mkuu Alhamisiwatakapokutana na Lebron James na Miami Heat.
Posted in Uncategorized on February 25, 2011 by sunday Shomari

Waandamamaji huko Libya wameweka hatua mpya ya kutaka kumwondoa madarakani kiongozi wao wa muda mrefu Moammar Gadhafi leo huku kukiwa na ripoti za mashambulizi ya risasi dhidi ya waandamanaji katika mji mkuu.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) mashirika ya habari yamewakariri waandamaanji wakisema majeshi yalio na uaminifui kwa Gadhafi yalifyatua risasi kwa waandamanaji waliotawanyika walioanza kuandamana huko Tripoli baada ya swala ya Ijumaa.
Wapinzani wa Gadhafi waliwataka wananchi kujitokeza katika mji mkuu baada ya swala.
Majeshi ya waasi yanasema yamechukua udhibiti wa mashariki mwa nchi na uungaji mkono wa vugu vugu la kupinga serikali linaongezeka magharibi ambapo zamani ndio kulikuwa ngome kuu ya Gadhafi.
Wanafunzi wa USIU-Kenya wafanya ziara VOA
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari
Wakiwa na zawadi zao baada ya ziara yao.

Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza akizungumza na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao wakimsikiliza mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza(hayupo pichani).
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari

Ndani ya Studio za Televisheni ya VOA.

Wakiwa kwenye Blue Carpet ya VOA.
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amewataka vikosi vyake vya usalama kuwalinda waandamanaji ambao wanamtaka ajiuzulu.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) shirika la habari la televisheni la Yemen, Saba news limetoa taarifa inayoeleza kwamba Bw. Saleh ameyataka majeshi ya usalama kuzuia mapigano yeyote kati ya waandamanaji wanaopinga serikali na wale wanaounga mkono.
Pia alizitaka pande zote mbili kuchukua tahadhari dhidi ya wale ambao watajaribu kuchochea waandamanaji na kuzidisha ghasia.
Kwa mara nyingine tena maelfu ya waandamanji wanaopinga serikali walimiminika katika uwanja mmoja katika mji mkuu wa Yemen San’aa.
Siku ya jumanne mtu mmoja aliuwawa na 12 kujeruhiwa wakati waandamanaji wa upinzani waliokusanyika katika chuo kikuu cha Sana’a kushambuliwa na watu walokua na bunduki na silaha nyenginezo walipojaribu kuwatawanya waandamanaji hao.
Kiasi ya wabunge saba wamejiuzulu kutoka chama tawala kulalamika dhidi ya utumiaji nguvu dhidi ya maandamano ya amani. Wabunge hao walieleza siku ya Jumatano kwamba wataunda kundi la wabunge wanaojitegemea bungeni.
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mh. Mwanaidi Sinare Maajar akiwa na Meya wa Jiji la Boise Mstahiki David Bieter pamoja na Afisa wa Ubalozi Suleiman Saleh na Rais wa Wafanya Biashara wa Jiji la Boise Bw. Connor katika ziara ya aina yake aliyofanya balozi Maajar akiwa ni balozi wa kwanza Tanzania kufanya ziara hiyo ambapo pia alikutana na watanzania waishio katika jimbo hilo.

Balozi Mwanaidi Maajar akikaribishwa rasmi na Meya David Bieter wa Jiji la Boise,Idaho ofisini kwake hivi karibuni.
Gadhafi adaiwa kuchukua mamluki
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari
Mashahidi katika mji mkuu wa Libya Tripoli wamesema mitaa mingi ilikuwa imebaki bila watu leo huku wakazi wakiogopa kutoka majumbani mwao siku moja baada ya kiongozi wa nchi hiyo Muamar Gadhafi kuwataka waunga mkono wake kuwashambulia waandamanaji wanaopinga serikali.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) mashahidi wameyaambia mashirika ya habari kwamba wafuasi waaminifu wa Gadhafi na mamluki kutoka nchi nyingine za Afrika walikuwa wanazunguka kwenye mji mkuu na kuwatisha watu wanaokaa kimakundi na kufyatua risasi hapa na pale.
Katika hotuba ya kwanza ya Gadhafi kwenye televisheni tangu upinzani dhidi ya utawala wake ulipoanza wiki iliyopita aliapa kubaki madarakani na kuwataka wafuasi wake kupambana dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali ambao aliwaita wahuni na magaidi. Ametishia kifo kwa yeyote atakayepambana dhidi ya Libya au kujihusisha na ujasusi.
Mugabe akamata wanaharakati 46
Posted in Uncategorized on February 24, 2011 by sunday Shomari
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani amesema rais Robert Mugabe hajajifunza kutokana na upinzani wa umma huko Misri na Tunisia .
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika msemaji P.J Crowley aliandika katika mtandao wa Twitter jumanne usiku .
Crowley alizungumzia kukamatwa kwa wanaharakati waliokuwa wamekutana kuzungumzia athari za upinzani huko Afrika ya kaskazini.
Polisi wa Zimbabwe walikamata watu 46 jumamosi na kuwashutumu kwa kula njama za kufanya maandamano kama yale yaliowaondoa viongozi wa Misri na Tunisia.



