Archive for December, 2010

Mambo ya mwaka mpya

Posted in Uncategorized on December 31, 2010 by sunday Shomari

KHERI YA MWAKA MPYA 2011.

Posted in Uncategorized on December 31, 2010 by sunday Shomari


Ni mwaka mwingine tena na hatimaye tunasema kwaheri kwa mwaka 2010 ni mwaka uliokuwa na mengi ya baraka na pia ya huzuni daima tutawakumbuka wale wapendwa wetu wote waliotutangulia kwenye haki.

Ni kazi ya mola na tunaendelea kumshukuru yeye kwa kila jambo katika maisha yetu ni vigumu kupokea lakini tumwombe Mungu atupe nguvu kuwakumbuka wale waliokuwa katika maisha yetu kama Baraka ya pekee na kuondoka kwao ama kwa hakika ni uchungu kwetu lakini pia tumshukuru Mola kwa muda mfupi tuliokuwa nao na tuangalie kwa upande wa chanya yale tuliyojifunza kutoka kwao.

Maisha ni mafupi binadam tunafahamu hatuwezi kuishi milele duniani kwahiyo kifo ni sehemu ya maisha yetu basi, tushangilie na kufurahia haya maisha ambayo tumepewa kwa sasa na pia tumshukuru yeye mwenyezi Mungu kwa kutupa pumzi na uhai kuuona huu mwaka mpya na tuuage mwaka uliopita kwa amani na si kwa ghasia na vurugu au matatizo.

Tuangalie ndugu zetu kule Ivory Coast hali ni tete angalia huko Somalia mabomu kila siku tupa macho kule Israel moto unawaka kila wakati, angalia huko Nigeria wakristo na waislam wanapambana nini dunia yetu inakokwenda? na je ukiwaambia watu wa huko washeherekee mwaka mpya watakuambiaje?

Mengi yametokea duniani ya kukumbukwa siwezi kuyataja yote hapa lakini tumejionea maajabu huko Chile wachimbaji madini walipotolewa chini ya ardhi ilikuwa ni kama kufukuliwa kaburini! Watu kadhaa waliokolewa hapa Marekani kutokana na dharuba ya theluji huko Maine na wengine kupoteza maisha. Huko Afrika wakati wa shamra shamra za kombe la dunia watu walipoteza maisha Kampala Uganda kwa shambulizi la bomu la Alshabab.

Ni mengi yametokea kwahiyo ukiwa unapumua hii leo ni wakati wa kufurahi kwa amani ,utulivu na usalama ghasia na ugomvi na chuki na wivu havitusaidiii kitu tuwe kitu kimoja , tupendane , kusameheana na kushirikiana , binaadamu tuna mapungufu yetu tukijua hili tutakuwa sawa. Wenzetu huko Asia wameshaanza kuuona mwaka mpya.

Kwa niaba ya Blog hii tunawatakia kheri ya mwaka mpya, nguvu mpya , kasi mpya , mafanikio makubwa zaidi, upendo, ushirikiano, maendeleo na kufanya yale yaliyo mema na bora zaidi na kumwomba mwenyezi Mungu atuzidishie mema katika mwaka wa 2011. Amen.

Posted in Uncategorized on December 31, 2010 by sunday Shomari

MAREHEMU SARA MAKAME HAJI

FAMILIA YA JULIUS NA FAITH KATANGA YA WASHINGTON DC, INAWAKARIBISHA MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA KATIKA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MDOGO WAO MAREHEMU SARA MAKAME HAJI ALIYEFARIKI DESEMBA 23,2010.IBADA HIYO ITAFANYIKA KATIKA KANISA LA CATHEDRAL OF PRAISE SAA 8:30 (2:30PM).TAFADHARI TUZINGATIE MUDA.

ANUANI
10110 GREENBELT ROAD
LANHAM,MD 20706

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA

JULIUS KATANGA 202 580 4648
MARCO MBULU 571 426 7124
TINO MALINDA 240 338 4917

WOTE MNAKARIBISHWA
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LITUKUZWE

Mambo ya mwaka mpya DMV

Posted in Uncategorized on December 31, 2010 by sunday Shomari

Mwanariadha maarufu Kenya kizimbani

Posted in Uncategorized on December 30, 2010 by sunday Shomari

Samuel Wanjiru


Bingwa wa Olimpiki Samuel Wanjiru amefikishwa mahakamani nchini Kenya na kufunguliwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe Teresia baada ya kumtolea bunduki ambayo anaimiliki kinyume cha sheria. Wanjiru ambaye pia ni mshindi mara mbili wa mbio za masafa marefu ya Boston alishtakiwa kwa kuwa na silaha kinyume cha sheria mbali na kutishia kumuua msaidizi wake wa nyumbani Bi. Nancy Njoki na pia kumjeruhi mlinzi wake William Masinde.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) Bw.Wanjiru wakati akigombana na mkewe mlinzi wao wa nyumbani alikuwa akijaribu kuzuia na ndipo alipojeruhiwa na Bw. Wanjiru lakini hata hivyo Wanjiru alikana mashtaka hayo mahakamani na kuachiliwa kwa dhamana ya shilling laki tatu za kenya.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa Wanjiru alifanya uhalifu huo usiku wa jumatano katika mtaa wa Muthaiga mjini Nyahururu lakini Bw. Wanjiri ni anaelezewa kuwa ni kijana mstaarabu anayeheshimika sana nchini Kenya kwa umaarufu wake na tabia zake kuonekana si mbaya kwa hiyo ni kitendawili kikubwa kwa wananchi nchini humo kutokana na tafrani hiyo, kesi yake imeahirishwa hadi January mwakani.

Maneno ya kukumbukwa 2010.

Posted in Uncategorized on December 30, 2010 by sunday Shomari


Mwenyekiti wa CUF Dr.Ibrahim Lipumba.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Rais wa pili wa Kenya Daniel Arap Moi.
Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) Esther G. Ewart alikusanya baadhi ya maneno ya viongozi na wanaharakati ambayo kwa hakika yatakumbukwa kwa mwaka 2010 kama ifuatavyo.


Rais wa Sudan atoa kitisho.

Posted in Uncategorized on December 30, 2010 by sunday Shomari

Rais Omar Hassan-al-Bashir


Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema nchi yake itajitoa kutoka mazungumzo ya amani ya Darfur huko Qatar na kupanga mazungumzo yake binafsi, kama hakuna maafikiano ya haraka ya mkataba na waasi.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika(VOA) Bwana Bashir aliuambia mkusanyiko wa wafuasi wake huko Darfur, Jumatano kwamba ujumbe wa Sudan utaondoka Doha na kufanya mazungumzo huko Darfur kama hakuna mkataba wowote. Pia alitishia majibu ya kijeshi dhidi ya mtu yeyote ambaye atanyanyua silaha huko Darfur.

Maafisa huko Khartoum hivi karibuni wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kuelekea kura ya maoni ya Januari 9, ambayo huwenda ikapelekea Sudan Kusini kuwa taifa huru, lakini makundi makuu ya uasi huko Darfur bado yanapigana na majeshi ya serikali. Mapigano ya wiki za hivi karibuni yamesababisha zaidi ya watu 10,000 kukimbia nyumba zao.

Wasanii waliotamba 2010 : Rita na Marlow

Posted in Uncategorized on December 29, 2010 by sunday Shomari

Katika kipindi hiki cha sherehe za mwisho wa mwaka tunaangalia baadhi ya wasanii waliotamba katika mwaka wa 2010.

Mmojawapo ni kijana machachari Marlow hiki ni kibao chake Rita.

George Clooney na Google ndani ya Sudan Kusini

Posted in Uncategorized on December 29, 2010 by sunday Shomari

George Clooney

Shirika moja lililoanzishwa na mcheza filamu wa Marekani George Clooney limesema limeungana na mtandao wa Google katika kutumia teknolojia ya satellite  ili kufuatilia kwa karibu uwezekano wa uhalifu wa kivita kabla ya kura ya maoni ambayo inaweza kuigawa nchi hiyo katika nchi mbili.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) shirika hilo la Clooney kwa jina Not On Our Watch limesema juhudi hizo  za kutumia mradi  wa Satellite zitatoa mpango maalum wa onyo la mapema kabla ya kura ya maoni ya  Sudan Kusini Januari 9 juu ya kujitenga na kuwa taifa huru au kubaki kama shemu ya Sudan.

Shirika hilo linasema litachukua picha za satellite ambazo zitaonyesha matembezi ya vikosi , raia na ishara nyingine endapo kutatokea mzozo kati ya upande wa kaskazini na kusini.

DUKA LA MTANDAO

Posted in Uncategorized on December 29, 2010 by sunday Shomari

Habari njema kwa Ndugu zangu Watanzania mnaoishi nje ya Tanzania, Tumefungua Duka la Mtandao(Onlineshop) la kuuza Chai na Kahawa ya Tanzania tuu. linaitwa Chai & kahawa Online Shop(www.chaikahawa.com) na liko Stockholm, Sweden.tunaweza kuuza na kusambaza chai na kahawa kwa mteja yeyote aliyopo nchi yeyote duniani. wote mnakaribishwa Kununua na kujivunia bidhaa zetu.

Kwa Mawasiliano,Maoni,Ununuzi wasiliana nasi kwa kutumia email info@chaikahawa.com au piga simu,tuma ujumbe mfupi(sms) + 46762878341.

NB:website iko kwenye Flash, kama utapata tabu kuifungua download flash adobe.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,705 other followers