Archive | August 7, 2010

Je Al Shabab wataweza kumalizwa?

Kundi la Alshabab

Kundi la Alshabab

Kitisho cha kundi la wanamgambo la Somalia Al Shabab chenye mahusiano na Al qaeda kimethibitika kuwa si mchezo na huenda kikaleta utata mzito katika ukanda wa Mashariki wa Afrika.

Tayari kundi hilo limeshapeleka vitisho mbali mbali katika nchi za maeneo hayo kikiwaonya wasithubutu kushiriki katika jeshi la kulinda amani huko Somalia kwa kulipua mabomu mawili mfululizo katika jiji la Kampala siku ya fainali ya kombe la dunia.

Kundi hilo limetoa vitisho kadhaa na hatimaye Umoja wa Afrika umeamua kwa kauli moja kuwa wanajeshi wake wataweza kushambulia wale wa Al Shabab ikiwa watagundua kundi hilo linataka kufanya mashambulizi. Hayo ni mabadiliko makubwa kwani awali askari hao walikuwa wanaruhusiwa tu kujitetea ikiwa watakuwa hatarini na sio kufanya mashambulizi.

Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mwanasheria wake mkuu Eric Holder aliyekwenda Uganda kumwakilisha Rais Obama kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) imesema iko tayari kuisaidia Afrika kwa vifaa na silaha na utaalam kupambana na waasi hawa hatari wa Al Shabab. Lakini ni wazi kuwa Marekani haitokaa ipeleke majeshi Somalia na ndio maana Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda alitoa ushauri wa wazi na kauli ya kijasiri kwamba Afrika lazima iamke na kupeleka majeshi kusaidia serikali ya Somalia.

Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona wazi hilo halitawezekana kwani nchi za Afrika zina matakwa tofauti na hali kila moja akiangalia ustaarabu wake ukiachilia mbali hali mbaya ya uchumi inayogonga nchi nyingi za Afrika, mpaka sasa ni Guinea pekee iliyotangaza kuongeza majeshi huko Somalia ambako tayari Uganda na Burundi wanayo majeshi yao.

Na kama mjuavyo Alshabab tayari wameshatoa onyo kwa nchi zipelekazo majeshi huko walipoanza kwa kuwalipua wananchi wa Uganda, lakini ni wazi nchi za Afrika inabidi ziamke na kuacha kutegemea misaada ya Marekani na nchi za Ulaya hasa inapokuja kwenye suala nyeti la usalama.

Nchi jirani ya Kenya tayari imeshatangaza kujiweka katika hadhari na kuwaangalia kwa makini raia wa Somalia nchini humo ambao wanasemekana wananunua  nyumba za fahari  kama karanga huku wakilipa fedha taslim na tena ni dola wala si fedha za nchini humo.

Kwa kiasi fulani hawa jamaa wanahusishwa na biashara haramu ya uharamia maana kwa nchi isiyo na mapato rasmi wananchi wake, fedha hizo wanazipata wapi au kwa kufanya biashara gani? na hawa wanajeshi wa kundi la Alshabab vifaa na silaha za kuwawezesha kupambana kila siku wanazitoa wapi? na fedha za kujikimu je? kazi ipo viongozi  Afrika kaeni macho.

Reality shows zinatufundisha nini?

Jerseyliciuos

Jerseyliciuos

JerseyShore

JerseyShore

real house wives of Dc

real house wives of Dc

Wamarekani wengi hivi sasa wanaganda kwenye runinga zao wakiangalia “Reality shows” filam zinazohusu maisha halisi ya wachezaji au waigizaji wake ama kwa hakiaka wakina dada wa Kardashians na T.O, bila kumsahau Ocho Cinqo na The girls next door, Ameriaca got Talent, Cham School,American Idol, The Bachelor, The Biggest Looser, For the Love of Ray J, KRuns House ,The Housewives of Atlanta,Dc n.k   na nyinginezo nyingi zimegusa maisha ya wananchi kwa hali ya juu.

Lakini wachambuzi wengi wamekuwa wakijiuliza je filam hizi zinaifunza jamii kitu gani au wananchi wanafaidika kweli na kutazama maisha ya watu ya kila siku? Lakini kuna kitu maana baadhi ya show hizi kwa kweli zimebadilisha maisha ya watu kwa mfano American Idol, washindi wa show pamoja na wale washiriki wanaofika mbali ama kwa hakika wanapata mikataba ya kufanya mambo mbali mbali ukiacha kurekodi muziki, kama vile filam kama Jennifer Hudson, Kucheza Opera New York Fantasia Borrino, na wale washindi kama vile wa Apprentice kujipatia kazi kubwa .

Lakini wakati huo huo show nyingine zinaonyesha maisha ya kila siku ya macelebrity kama Kardashians je yanasaidiaje watu kwa wale wapenda kujua maisha ya watu hasa macelebrity hizi show ndio haswa wamefika ili wajionee leo kina Kardashian wamevaa nini? au wamesema nini na ama kwa hakika masupa staa hawa wanapata ufuatiliaji wa kila aina kutoka kwa wananchi mbali mbali kujionea kila jambo wanalofanya na hii ndio inamfanya kila staa aanzishe kitufulani .

Kwasababu watu wana kiu ya kujua hawa jaama aa wanaishije, wakati huo huo  Steve Harvey akizungumza katika moja ya shughuli zake za kuchekesha alisema “sisi wote tuko sawa” kama watu wengine ila tu tulipata hela zaidi lakini msisahau sisi ni watu wa kawaida kama wengine”.

Real House wives of Dc inaanza na tayari kuna mazungumzo mengi kuhusu show hiyo ikiwa na mwanamke maarufu aliyevamia party ya white house bila kualikwa Michaela Solahi tayari vyombo vya habari vinazungumzia ujio wa show hii na wananchi mbali mbali wametoa maoni yao wengine wakidai hawana haja nayo kwasababu  mama huyu na vitendo vyake vya kupenda umaarufu anawachosha.

Wakati huo huo alipambana vikali na Whoopi Goldberg kwenye kipindi maarufu cha “The View” ambapo mama huyu mwenye drama alidai Whoopi kampiga na kumsema vibaya na kumshushia hadhi yake kwa kumwita Party Crasher na pia mtangazaji mwingine Sherri Shepherd kamwambia anastahili kuwa jela.

Whoopi amedai aliongea maneno ya kawaida ila mume wake aliyekuwa akimpiga picha bila ridhaa yake alimfanya awape maneno ya kuchagua namnukuu “choice words”. Na kwa ujumla alidai alimgusa mama huyu ili ajibu swali alokuwa ameulizwa wakati wa mahojiano na si kumchokoza.

Kazi ipo hizi Reality show zinapendwa mno na baadhi ya watu sababu wanataka kujua maisha ya watu wengine hasa macelebrity kwahiyo nionavyo mimi zitaongezeka kila siku mradi zina watazamaji bila kujali wanajifunza mema au mabaya na alimradi wamiliki wa vyombo vya habari wanatengeneza fedha yao. Kazi iko.