Archive for August, 2010

Miss Universe 2010 atokea Mexico

Posted in Uncategorized on August 25, 2010 by sunday Shomari
Miss Universe Jemina Navarrete

Miss Universe Jemina Navarrete

Miss Universe katika vazi la kuogelea

Miss Universe katika vazi la kuogelea

Mwanadada mrembo wa Mexico Jimena Navarrete ndiye ameibuka mshindi wa Miss Universe 2010 huko Las Vegas Nevada baada ya kuwatoa washiriki wengine kutoka nchi 82 duniani.

Kimwana huyo mwananana mwenye umri wa miaka 22 alishinda kwenye kinyang’anyiro cha mavazi ya kuogelea na vazi la jioni. Mrembo huyu alijipatia pointi nyingi katika kipindi cha maswali baada ya kujibu vyema swali kuhusu  wazazi wanaowaachia watoto kutumia mtandao bila  usimamizi wowote. Dada huyu alijibu kwa kupitia mkalimani kwamba mtandao ni chombo muhimu sana kwa sasa na hakiwezi kuachwa lazima tuhakikishe tunawafundisha maadili tuliyojifunza kama familia.

Majibu haya yalimpa nafasi kimwana huyu amnbaye alikuwa nyuma ya kimwana wa Phillipines ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya ushindi lakini alijikuta akiishia nafasi ya nne baada ya kushindwa kujibu vyema swali aliloulizwa. Swali lilikuwa ni kuhusu makosa gani aliyofanya maishamni mwake lakini aliishia kucheka na kusema Asante kwa nafasi hii na sikumbuki makosa yeyote maishani mwangu.

Rais wa Mexico Felipe Calderon alituma salam za pongezi kwa mrembo huyo wa nchi yake kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yake. Miss Mexico Jemina Navarrete amechukua taji kutoka kwa Stefania Fernandez Miss Venezuela ambaye alikuwa mshindi wa 2009.

Mshindi huyu wa Miss Universe atapata makazi katika nyumba ya fahari New York ambayo analipiwa kwa mwaka mzima, mshahara ambao haujatajwa, gharama zake zote zinalipwa, vito vya thamani, nguo na viatu kwa mwaka mzima na scholarship ya masomo huko New York Film Academy pamoja na malazi mara baada ya muda wake kumalizika.

Mashindano haya yanaandaliwa kwa pamoja kati ya Donald Trump na NBC TV. Chanzo cha habari yahoo!news

Miss Universe katika vazi la jioni

Miss Universe katika vazi la jioni

Miss Universe katika pozi

Miss Universe katika pozi

Pakistan maafa ni makubwa mno kuzidi majanga yaliopita

Posted in Uncategorized on August 23, 2010 by sunday Shomari
Mafuriko ya Pakistan

Mafuriko ya Pakistan

Nchi ya Pakistan imekumbwa  na mafuriko mabaya kuliko yote katika historia ya nchi hiyo kwa mujibu wa Umoja wa mataifa  mafuriko hayo yameleta maafa makubwa kuliko tsunami kwenye bahari ya Hindi 2004, tetemeko la Kashmir 2005 na tetemeko la Haiti 2010 kwa pamoja.

Lakini wachambuzi wanaeleza ni kwa nini  pengine inafikiriwa kama vile  mafuriko haya si makubwa kama ilivyokuwa majanga haya mengine na wameeleza kuwa ni  kutokana na idadi ya watu waliokufa kuwa ni ndogo kuliko hayo majanga mengine.

Lakini kwa mujibu wa Umoja wa mataifa  mafuriko haya ni makubwa sana  kwasababu mpaka sasa idadi ya walioathirika ni kubwa mno  na inaripotiwa  kuwa wanawake wajawazito pekee ni   laki 5  ambao hawana makazi mpaka sasa na karibu watu milioni 13 kwa jumla hawana mahali pa kuishi. Idadi ya vifo inakadiriwa kuwa 1500 mpaka sasa.

Watu wengi wanalala kwenye miti na mahema na wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe. Nchi hii inahitaji msaada mkubwa kwa kweli. Mpaka sasa Marekani imeahidi kutoa dola milioni 150 kusaidia nchi hiyo, lakini hali ya misaada bado inasemekana ni ndogo sana na inapatikana kwa taratibu sana kwani inachukua muda mrefu kuwafikia walengwa.

Mayai hatari Marekani! tuwe macho

Posted in Uncategorized on August 22, 2010 by sunday Shomari

Shirika la usimamizi na ukaguzi wa chakula la Marekani (FDA) limetangaza hivi karibuni kuwa mayai yatengenezwayo na mashirika kadhaa hapa Marekani yana vijidudu vya Salmonela. Ugunduzi huo umepelekea shirika hilo kuagiza kuondolewa sokoni kwa mayai takriban nusu bilioni.

Kwa mujibu wa shirika hilo Wamarekani wanakula mayai milioni 220 kwa siku, shamba moja lililopo huko Iowa- Hilandale Farms limeondoa sokoni mayai yapatayo milioni 170 baada ya zaidi ya watu 1000 kuugua huko Iowa na majimbo mengine matatu. Waatalam wanaeleza kuwa uzalishaji wa mayai wa shirika moja pekee unaweza kusababisha watu kadhaa hapa Marekani kuugua na mpaka sasa shamba hilo  la  Hillandale Farms ni la pili kusimamisha uzalishaji wa mayai yake na kuondoa yaliopo madukani.

Inashauriwa kula mayai yaliopikwa na  yakaiva vizuri kwani ndio yanaweza kuuwa vijidudu, mayai kama jicho la ng’ombe ambalo halijaiva vizuri au la kukaanga ambalo lina rojo rojo au chips mayai iliyorojorojo ni hatari sana kwa wakati huu.

Ugonjwa unaotokana na vijidudu hivi unaweza kuuwa watoto na wazee na wale walio na chembe chembe  za kulinda mwili dhaifu kwa urahisi sana na dalili zake ni kichefu chefu, kuharisha ambako kunaweza kuwa na damu, maumivu ya tumbo na homa.

Watu 2000 katika majimbo mbali mbali  wameripotiwa kuugua mpaka sasa kutokana na vijidudu vya Salmonela vilivyotoka kwenye mayai hayo, ushauri wa bure ni  kuwa bora kutupa mayai uliyonayo hasa ukiwa hujui ni shirika gani linahusika  na kuachana na mayai kwa sasa mpaka hali itakapodhibitiwa. Lakini utajuaje mayai yapi hayafai? Shirika la usimamizi wa chakula limetoa orodha ya mayai kutoka mashirika yanayohofiwa kuwa na Salmonela kama ifuatavyo. Brand ikiwa ni aina ya mayai ikifuatiwa namba ya kiwanda na  tarehe ya Julian.

Brand Plant Number Julian Dates
Albertson
1413
136 through 225
Albertson
1026
136 through 225
Albertson
1720
136 through 229
Albertson
1942
136 through 229
Bayview
1686
142 through 149
Boomsma’s
1413
136 through 225
Boomsma’s
1946
136 through 225
Boomsma’s
1720
136 through 229
Boomsma’s
1942
136 through 229
Country Eggs
1026
216 through 221 (15-dozen bulk)
Country Eggs
1946
216 through 221 (15-dozen bulk)
Dutch Farms
1946
136 through 225
Farm Fresh
1026
136 through 225
Farm Fresh
1946
136 through 225
Farm Fresh
1720
136 through 229
Farm Fresh
1942
136 through 229
Glenview
1720
136 through 229
Glenview
1942
136 through 229
Hillandale
1413
136 through 225
James Farms
1720
136 through 229
James Farms
1942
136 through 229
Kemps
1946
136 through 225
Kemps
1720
136 through 229
Kemps
1942
136 through 229
Lucerne
1413
136 through 225
Lucerne
1026
136 through 225
Lucerne
1946
136 through 225
Lund
1946
136 through 225
Lund
1720
136 through 229
Lund
1942
136 through 229
Mountain Dairy
1951
193 through 208
Mountain Dairy
1413
136 through 225
Mountain Dairy
1026
136 through 225
Mountain Dairy
1720
136 through 229
Mountain Dairy
1942
136 through 229
Nulaid
1091
167 through 174
Nulaid
1951
195 through 210
Pacific Coast
1720
136 through 229
Pacific Coast
1942
136 through 229
Ralph’s
1413
136 through 225
Ralph’s
1026
136 through 225
Ralph’s
1720
136 through 229
Shoreland
1026
136 through 225
Sunny Farms
1860
099 through 230
Sunny Farms
1663
137 through 230
Sunny Meadows
1860
099 through 230
Sunny Meadows
1663
137 through 230
Sunshine
1413
136 through 225
Sun Valley
1951
195 through 209
Trafficanda
1413
136 through 225

Au pakiti ya mayai hayo inaonekana kama hivi ikiwa na namba ya kiwanda na tarehe:

Lebo za mayai hayo

Lebo za mayai hayo

-

Je Tea Party wataweza kumwangusha Obama?

Posted in Uncategorized on August 18, 2010 by sunday Shomari
Rais wa Marekani Barack Obama

Barack Obama

Suala la vugu vugu la Tea Party limeleta sura mpya kwenye siasa za Marekani ambapo katika siku za karibuni vugu vugu  hilo limechukua nafasi ya pekee katika siasa za Marekani na hasa kumpinga Rais Barack Obama na sera zake kuanzia mabadiliko ya afya mpaka ya mfumo wa fedha na shutuma mbali mbali ikiwa ni pamoja na kumwita mjamaa na asiye raia wa Marekani. Si hivyo tu walikampeni dhidi ya Obama na wagombea wake katika nafasi mbali mbali kiasi cha kwamba Chama cha Democrat kilipoteza jimbo muhimu lililobadili msimamo kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 la Virginia  kutoka Republikan na kumchagua Obama Mdemocrat ambapo Gavana wa jimbo hilo alirudi kuchaguliwa Mrepublikan na si hivyo tu hayo  hayakuishia hapo  yalienda New Jersey ambapo lile ni jimbo la wademocrat lakini la hasha walijikuta wakilipoteza kwa warepublikan ambapo alichaguliwa  Gavana mrepublikan Chris Christie pamoja na kampeni kali za Obama.

Sasa kutokana na hayo  nimezungumza na mtafiti na mchambuzi  wa kisiasa na mfasiri wa kujitegemea Professa John Mtembezi na kumuuliza kama Je vugu vugu hili litaweza kumwangusha Rais Barack Obama kwenye uchaguzi wa mwaka 2012. Na Profesa anaeleza yafuatayo:

Profesa John Mtembezi

Profesa John Mtembezi

Kuhusu Tea Party na uwezo wake wa kumwangusha Obama 2012, mimi binafsi sidhani wao peke yao wataweza kufanya hivyo. Kwanza tukumbuke kuwa Tea Party ni mseto wa watu kadhaa wenye itikadi, siasa, na mtazamo wa dunia nzima vinavyolingana. Lakini Tea Party yenyewe si chama cha siasa. Wengi wao hujiita “Marepublican” isipokuwa mara nyingi watu hao hao ndio wanaopinga vikali baadhi ya sera za chama cha Republican pamoja na wanasiasa wa chama hicho. Hivyo, vuguvugu lao la kisiasa, kwa kiasi kikubwa, ni kama uasi ndani ya chama cha Republican. Hivyo, upo uwezekano harakati za vuguvugu hilo zitahatarisha wanasiasa wa chama hicho kuchaguliwa tena mwezi wa Novemba.
Vilevile kupinga sera fulani fulani ni kazi rahisi; lakini kupendekeza ya kufanya ili kurekebisha hali fulani na halafu kulitekeleza pendekezo hilo ni tofauti na ni kazi ngumu zaidi.
Tuangalie masuala makuu mawili yaliyo muhimu sana kwao. La kwanza ni lile la ndoa ya watu wa jinsia moja. Nakubali kwamba walio wengi nchini humu hawapendi kuona ndoa za namna hiyo zifanywe halali. Lakini tusisahau kwamba haizidi miaka 25 iliyopita watu wengi nchini huku hawakupeda pia kuona ndoa baina ya mweusi na Mzungu, wengine wao wakidai eti ndoa ya namna hiyo inakwenda kinyume na mila, desturi, na matakwa ya Mwenyezi Mungu!
Mstari wa kitako ni huu: watu wanaoitwa “gay” katika nchi hii … yaani wasenge na wasagaji … wamezaliwa hapa, wamekulia hapa, wengi ni walipaji kodi kama Wamarekani wengine, wengine ni wanasiasa, na wengine wamewahi kuwa hata wanajeshi nyakati za vita. Ikiwa ni hivyo, basi swali la kimsingi linalofuatia ni: “Je, wao ni wananchi halisi wa Marekani au la?” Kama jibu ni la, wao sio wananchi, basi nadhani wenye kujibu hivyo waona itakuwa sawa kuwanyima haki za kiraia na kuwabagua na kuwadhulumu. Lakini tukikubali ya kuwa hao ni raia halisi wa nchi hii, basi wao hawana budi kupatiwa haki zote za kiraia bila ya kubaguliwa. Kufanya vingine ni kukubali kuwa nchini huku kuna matabaka mawili ya uraia, walio wengi wasio wasenge au wasagaji na walio wachache walio “gay.”
Neno la mwisho ni hili: kutoa hoja kwamba misahafu kama vile Torati, Biblia, au Kurani kwa inasema mwenendo huo dhambi ni kukiuka katiba ya Marekani inayosema bayana kabisa kwamba hakuna dini rasmi ya serikali au nchi na kwamba uhuru wa kuabudu (au kutoabudu) dini yoyote ni haki isiyopingika.
Suala la pili ambalo linatawala akili za wengi wa Tea Party ni kodi. Hawapendi kodi. Walakini iwapo kodi ni kitu cha lazima, basi ziwe ndogo sana, hasa kwa sekta ya biashara na watu walio matajiri. Tukipiga darubini msimamo huu tutagundua kuwa serikali si kama kampuni. Haina bidhaa za kuuza wala haina hudumu za kutoa kwa malipo. Njia kuu kwa serikali ya kidemokrasia ya  kujipatia pesa za kuendelezea nchi ni kwa kukusanya kodi kutoka kwa wananchi wote, maskini kwa matajiri, pamoja na makampuni na mashirika. Pasipo kodi serikali itawezaje kuboresha miundo mbinu ya nchi ili kufanya ukarabati madarajani, mabarabarani, n.k? Itawezaje kujenga mashule au kuinua hali ya elimu nchini? Itawezaje kulipa mishahara ya askari polisi, wazima moto, wanajeshi, walimu, na watumishi wa serikali? Bila kodi, au kodi za kutosha, nchi ingesambaratika katika hali ya vurugu tupu.

Ubaguzi wa rangi ungali upo kwenye jamii ya Kimarekani hivyo lazima wengi kama si wote wa wana-Tea Party ni wabaguzi wa rangi, hata kama wako weusi wachache waliojiunga na vuguvugu hilo. Hili si jambo geni. Kihistoria na katika nchi zote kumekuwa na watu waliorubuniwa akili zao au waliojifikiria nafsi zao tu. Mathalan, enzi ya utumwa nchini huku kulikuwa na watumwa wengi waliowasaliti watumwa wenzao kwa kufichua mipango ya kutoroka ya watumwa wengine.

Na kuhusu suala la mgombea wa chama cha demokrat katika nafasi ya useneta huko South Carolina Mark Green ambaye ametokea kushinda kiajabu nafasi ya kuwa mgombea wa chama hicho jimboni humo nini mtazamo wa Profesa John Mtembezi?

Juu ya Mark Green sijui mengi kuhusu maisha yake na siasa zake. Nimesikia kuwa amekuwa na matatizo fulani na polisi na kwamba kabla ya kugombea ubunge wa South Carolina hali yake ya kiuchumi haikuwa nzuri. Sasa watu wajiuliza aliwezaje kupata 10,000 pesa za kimarekani kujiandikisha apate kugombea uchaguzi huo. Na pesa za kuendeleza kampeni yake nazo zikatoka wapi? Nimewahi kumsikia akiongea kwenye mahojiano ya redio na yeye si mbumbumbu, akili anazo za kutosha. Lakini bado yapo maswali na tuhuma juu yake. Chama cha Democrats hakimwungi mkono kikamilifu kikiamini kwamba yeye hawakilishi maslahi ya Mademocrats bali amekula njama na chama cha upinzani. Mademocrats wengi waamini Richard Green akiwa mgombea anayewakilisha chama chao kugombea kiti cha ubunge mwezi wa 11, atashindwa kwa urahisi na mgombea wa chama cha Republican.

Mike Tyson aongelea mabadiliko ya maisha yake

Posted in Uncategorized on August 15, 2010 by sunday Shomari
Mike Tyson na mwanae

Mike Tyson na mwanae(Picha na Getty Images)

Mike Tyson pichani hivi karibuni alihudhuria pambano la Juan Marquez na Diaz huko Mandalay Bay Las Vegas akiwa na mwanae wa kike ambapo alipokuwa huko alifanya mahojiano na radio ya ESPN.

Katika mahojiano hayo waliongelea juu ya maisha yake baada ya kustaafu mchezo wa masumbwi na hasa matumizi ya madawa ya kulevya ambapo  alieleza hali ilikuwa mbaya sana na alishiriki kwenye filam ya Hangover ili aweze kupata fedha za madawa hayo na hakujua nini hasa kilimtokea mpaka akafikia hatua hiyo. Lakini hakutegemea filam hiyo ingekuwa na mafanikio makubwa iliyopata. Lakini hivi sasa Tyson  ameacha matumizi ya madawa hayo. Nao watengenezaji wa filam hiyo wanafikiria kutoa Part II ambayo pia huenda Jammie Fox akawemo kwa mujibu wa Mike Tyson.

Katika mahojiano hayo pia alizungumzia kuhusu uzito wake ambao sasa amepunguza kutoka paundi 300 hadi 215 akidai kwamba unene ulimpa shida sana na alipoulizwa kitu gani kilimpa taabu alijibu kwa utani huku akicheka kwamba hasa baada ya  kujisaidia shughuli ya usafi ilikuwa ni ngumu sana.

Aidha aliendelea kusema kuwa nguo anazovaa hivi sasa ni nguo alizokuwa nazo tangu miaka 15 hadi 20 iliyopita. Na pia alielezea amejifunza kupenda na kusamehe wakati wa Hija huko Mecca na  kuhusu wanawake wazuri duniani alisifia kina dada wa Russia akidai aliona raia wa Russia weusi wazuri sana na hapo hapo aliongezea chachandu kwa kuwatania kina dada wa  Afrika na Haiti kuwa wana mambo ya kishirikina mno.

Amehamia Las Vegas Nevada kwa sasa lakini amesema kuwa mkewe bado anaishi New York  kwani hapendi kuishi  Las Vegas na kuhusu muziki amesema hajui chochote kuhusu miziki ya Hip hop kwa sasa inaonekana amebadili   maisha yake kwa kiasi fulani.

Kila la kheri mwakilishi wa Tanzania kwenye Miss Universe!

Posted in Uncategorized on August 14, 2010 by sunday Shomari
Miss Universe Tanzania alipokata tiketi ya michuano hiyo Tanzania

Miss Universe Tanzania alipokata tiketi ya michuano hiyo Tanzania

Hellen Dausen mwakilishi wa  Tanzania katika shindalo la 59 la Miss Universe hapa Marekani atapeperusha bendera ya Tanzania kwenye shindano hilo ambalo litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya NBC Agosti 23,2010 hapa Marekani.

Washiriki wa shindano hilo hivi sasa tayari wameanza kupewa alama  zao za  juu zikiwa kwa wale wanaoonekana kuwa na uwezo wa kufanya vyema kwenye shindano hilo litakalofanyika huko Mandalay Bay Las Vegas.

Hivi sasa nyota zimeanza kuonekana miongoni mwa washiriki ambapo alama za juu mpaka wakati huu zinashikiliwa na Mwakilishi wa  Phillipines  Venus Raj akiwa na pointi 3.74 naye mwakilishi wa Afrika mwenye alama za juu kidogo ni mwakilishi wa Ghana Awurama Simpson akiwa na pointi 2.53 naye mwakilishi wa Tanzania Hellen Dausen anazo pointi 1.95.  Mashindano haya yanashirikisha wananchi kutoka nchi 83 duniani.  Kila la kheri Hellen Dausen.

Miss Universe Tanzania yuko Las Vegas akiwakilisha Tanzania

Miss Universe Tanzania yuko Las Vegas akiwakilisha Tanzania

Je Dr Slaa ni tishio kwa CCM?

Posted in Uncategorized on August 14, 2010 by sunday Shomari
Mgombea wa Chadema Dr.Wilbroad  Slaa

Mgombea wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa

Chama tawala nchini Tanzania cha CCM kimeonekana au kuonyesha kumzungumzia mgombea urais wa upinzani na katibu mkuu wa chama cha Chadema Dr.Wilbroad Slaa. Hii imetokana na mgombea wa chama tawala Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  J.K kutoa onyo kwa chama hicho kutobweteka na kuwa macho na wapinzani akimtaja Dr.Slaa.

Wachambuzi wa siasa za Tanzania wanachojiuliza ni kwamba mbona wagombea wengine hawakutajwa isipokuwa Dr.Slaa? mgombea huyu wa urais kupitia Chadema alikuwa mmoja wa wabunge machachari waliotoa hoja nzito sana bungeni na zilizowapa taabu viongozi wa chama tawala ikiwa ni pamoja na orodha ya mafisadi.

Mgombea huyu ambaye alikuwa ni mbunge wa Karatu kwa kupitia Chadema yeye na chama chake wameomba mdahalo na wagombea wengine wa urais lakini chama tawala kupitia katibu mkuu wake Bw.Yussuf Makamba  kimeeleza kutokuwa tayari kwa mgombea wao rais wa jamhuri ya muungano kushiriki, Chadema tayari wameshatoa maelezo kwamba katibu mkuu wa chama tawal Yussuf Mkamba anaogopa mgombea wake rais wa jamhuri ya muungano kupambana nao kwenye mdahalo kwani tayari Dr.Slaa akiwa na orodha ya mafisadi 11  atadai majibu kwa rais ambayo inaweza ikawa ngumu kwa rais kujibu.

Katika karne hii ya 21 kampeni za uongozi za kila nchi iliyoendelea zinakwenda sambamba na midahalo ya wagombea kwani hiyo inawapa wananchi nafasi ya kufahamu zaidi wagombea wao wana sera gani na si hivyo tu wakati wa 2005 nchini Tanzania mdahalo ulifanyika kati ya wagombea urais wa wakati huo.

Je lipi ni la ajabu leo  hii kwamba chama tawala hakitaki kufanya mdahalo? Rais Kikwete amekuwa akitumia vyombo vya habari na mtandao pale alipofanya mahojiano na wananchi kupitia TvT na kuonyesha kuwa Rais mwenye nia ya kuwa wazi mbele ya wananchi wake sasa leo imekuwaje?  mpaka chama chake kinakataa kufanya mdahalo?

Chadema wakisema kwamba kuna mambo wanayoficha je watapinga na kwa hoja gani? sikuzote mdahalo unawapa wananchi nafasi ya kujionea wagombea wakishindana kwa nguvu za  hoja na  katibu mkuu wa CCM huu ni wakati wa kuwa wazi na kufanya mdahalo ili wananchi wapate nafasi ya kuwasikia viongozi wao wakishindana kwa hoja, tatizo liko wapi mbona Mkapa alikubali kufanya mdahalo 1995?

Chama cha  ccm na Chadema vimeshutumiwa kufanya kampeni mapema kabla ya wakati wake na baadhi ya vyama vya upinzani vikimtaka msajili wa vyama John Tendwa achukue hatua. Kampeni zinatakiwa kuanza rasmi Agosti 20 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wa Tanzania. Katika kile walichodai ni kuomba udhamini kwa wananchi wagombea hawa wa CCM na Chadema wamekuwa wakipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi kitu ambacho wenzao wamedai ni kampeni za mapema kwa hiyo waonywe au kuenguliwa kugombea lakini hilo linawezekana kweli?

Dr Slaa akiwasilimia wafuasi wake kwenye moja ya mikutano

Dr Slaa akiwasilimia wafuasi wake kwenye moja ya mikutano

Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Tiger Woods?

Posted in Uncategorized on August 9, 2010 by sunday Shomari
Tiger Woods

Tiger Woods

Mcheza golf mashuhuri Tiger Woods na mchezaji mwenye kipato cha juu kuliko wachezaji wengine wote duniani amekumbana na kigigingi kingine baada ya kufanya vibaya kuliko mechi nyingine zote tangu aanza kucheza mechi za kulipwa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun  mchezaji huyo yuko chini kabisa hivi sasa baaada ya matokeo hayo mabaya na kumpa nafasi mpinzani wake Jack Nicklaus kuweza kuchukua nafasi ya juu katika mashindano ya mashindao ya Ryder Cup na yale yajayo ya PGA tour.

Tiger woods baada ya kupata kashfa ya ngono amepoteza matangazo kwa asilimia 86 kiasi cha dola milioni 122 kwa mwaka 2010 lakini pamoja na hayo yote bado anakamata nambari moja katika malipo miongoni mwa wanamichezo.

Tiger mwenye umri wa miaka 34 amesema alijitahidi na kuwa mtulivu wakati wa michuano hiyo lakini hiyo haikutosha anategemea kujiandaa zaidi kwa michuano ijayo ya PGA tour akisema anao muda wa kufanya vyema.

Kwa nini bado yupo Nike?

Pamoja na kashfa hizo kampuni kama Nike hazijamwacha Tiger Woods  na hiyo imetajwa kuwa huenda ni kwasababu mwanamichezo huyo ana hisa kwenye kampuni  hiyo na inasemekana Wamarekani wengi hawana tena mapenzi na yeye kama ilivyokuwa zamani.

Wanamchezo wengi na wanasiasa wanaharibiwa maisha na kashfa, ukiangalia yaliomtokea Tiger Woods Novemba mwaka jana juu ya kashfa ya kuwa na wanawake kadhaa nje ya ndoa yake yanaelekea kuwa sasa pengine  ndio yanamharibia Tiger uwezo wake wa kucheza.

Iliripotiwa Tiger Woods anatalikiana na mkewe lakini mengi yamesemwa lakini  karatasi za talaka bado hazijaonekana kwenye mahakama yoyote na zinasubiriwa kwa hamu na waandishi wa habari.

Lakini kwa ujumla kinachoendelea nje ya uwanja wa Golf kwa Tiger Woods hivi sasa kina athari mbaya kwake kwa hiyo kwa ujumla anahitaji kufanya kazi kubwa kurudi katika maisha yake ya kawaida kwani bado kuna mushker ambao haujulikani wazi.na imeripotiwa na ESPN kwamba hivi sasa Tiger Woods hana kocha kulikoni?

Je Al Shabab wataweza kumalizwa?

Posted in Uncategorized on August 7, 2010 by sunday Shomari
Kundi la Alshabab

Kundi la Alshabab

Kitisho cha kundi la wanamgambo la Somalia Al Shabab chenye mahusiano na Al qaeda kimethibitika kuwa si mchezo na huenda kikaleta utata mzito katika ukanda wa Mashariki wa Afrika.

Tayari kundi hilo limeshapeleka vitisho mbali mbali katika nchi za maeneo hayo kikiwaonya wasithubutu kushiriki katika jeshi la kulinda amani huko Somalia kwa kulipua mabomu mawili mfululizo katika jiji la Kampala siku ya fainali ya kombe la dunia.

Kundi hilo limetoa vitisho kadhaa na hatimaye Umoja wa Afrika umeamua kwa kauli moja kuwa wanajeshi wake wataweza kushambulia wale wa Al Shabab ikiwa watagundua kundi hilo linataka kufanya mashambulizi. Hayo ni mabadiliko makubwa kwani awali askari hao walikuwa wanaruhusiwa tu kujitetea ikiwa watakuwa hatarini na sio kufanya mashambulizi.

Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mwanasheria wake mkuu Eric Holder aliyekwenda Uganda kumwakilisha Rais Obama kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) imesema iko tayari kuisaidia Afrika kwa vifaa na silaha na utaalam kupambana na waasi hawa hatari wa Al Shabab. Lakini ni wazi kuwa Marekani haitokaa ipeleke majeshi Somalia na ndio maana Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda alitoa ushauri wa wazi na kauli ya kijasiri kwamba Afrika lazima iamke na kupeleka majeshi kusaidia serikali ya Somalia.

Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona wazi hilo halitawezekana kwani nchi za Afrika zina matakwa tofauti na hali kila moja akiangalia ustaarabu wake ukiachilia mbali hali mbaya ya uchumi inayogonga nchi nyingi za Afrika, mpaka sasa ni Guinea pekee iliyotangaza kuongeza majeshi huko Somalia ambako tayari Uganda na Burundi wanayo majeshi yao.

Na kama mjuavyo Alshabab tayari wameshatoa onyo kwa nchi zipelekazo majeshi huko walipoanza kwa kuwalipua wananchi wa Uganda, lakini ni wazi nchi za Afrika inabidi ziamke na kuacha kutegemea misaada ya Marekani na nchi za Ulaya hasa inapokuja kwenye suala nyeti la usalama.

Nchi jirani ya Kenya tayari imeshatangaza kujiweka katika hadhari na kuwaangalia kwa makini raia wa Somalia nchini humo ambao wanasemekana wananunua  nyumba za fahari  kama karanga huku wakilipa fedha taslim na tena ni dola wala si fedha za nchini humo.

Kwa kiasi fulani hawa jamaa wanahusishwa na biashara haramu ya uharamia maana kwa nchi isiyo na mapato rasmi wananchi wake, fedha hizo wanazipata wapi au kwa kufanya biashara gani? na hawa wanajeshi wa kundi la Alshabab vifaa na silaha za kuwawezesha kupambana kila siku wanazitoa wapi? na fedha za kujikimu je? kazi ipo viongozi  Afrika kaeni macho.

Reality shows zinatufundisha nini?

Posted in Uncategorized on August 7, 2010 by sunday Shomari

Jerseyliciuos

Jerseyliciuos

JerseyShore

JerseyShore

real house wives of Dc

real house wives of Dc

Wamarekani wengi hivi sasa wanaganda kwenye runinga zao wakiangalia “Reality shows” filam zinazohusu maisha halisi ya wachezaji au waigizaji wake ama kwa hakiaka wakina dada wa Kardashians na T.O, bila kumsahau Ocho Cinqo na The girls next door, Ameriaca got Talent, Cham School,American Idol, The Bachelor, The Biggest Looser, For the Love of Ray J, KRuns House ,The Housewives of Atlanta,Dc n.k   na nyinginezo nyingi zimegusa maisha ya wananchi kwa hali ya juu.

Lakini wachambuzi wengi wamekuwa wakijiuliza je filam hizi zinaifunza jamii kitu gani au wananchi wanafaidika kweli na kutazama maisha ya watu ya kila siku? Lakini kuna kitu maana baadhi ya show hizi kwa kweli zimebadilisha maisha ya watu kwa mfano American Idol, washindi wa show pamoja na wale washiriki wanaofika mbali ama kwa hakika wanapata mikataba ya kufanya mambo mbali mbali ukiacha kurekodi muziki, kama vile filam kama Jennifer Hudson, Kucheza Opera New York Fantasia Borrino, na wale washindi kama vile wa Apprentice kujipatia kazi kubwa .

Lakini wakati huo huo show nyingine zinaonyesha maisha ya kila siku ya macelebrity kama Kardashians je yanasaidiaje watu kwa wale wapenda kujua maisha ya watu hasa macelebrity hizi show ndio haswa wamefika ili wajionee leo kina Kardashian wamevaa nini? au wamesema nini na ama kwa hakika masupa staa hawa wanapata ufuatiliaji wa kila aina kutoka kwa wananchi mbali mbali kujionea kila jambo wanalofanya na hii ndio inamfanya kila staa aanzishe kitufulani .

Kwasababu watu wana kiu ya kujua hawa jaama aa wanaishije, wakati huo huo  Steve Harvey akizungumza katika moja ya shughuli zake za kuchekesha alisema “sisi wote tuko sawa” kama watu wengine ila tu tulipata hela zaidi lakini msisahau sisi ni watu wa kawaida kama wengine”.

Real House wives of Dc inaanza na tayari kuna mazungumzo mengi kuhusu show hiyo ikiwa na mwanamke maarufu aliyevamia party ya white house bila kualikwa Michaela Solahi tayari vyombo vya habari vinazungumzia ujio wa show hii na wananchi mbali mbali wametoa maoni yao wengine wakidai hawana haja nayo kwasababu  mama huyu na vitendo vyake vya kupenda umaarufu anawachosha.

Wakati huo huo alipambana vikali na Whoopi Goldberg kwenye kipindi maarufu cha “The View” ambapo mama huyu mwenye drama alidai Whoopi kampiga na kumsema vibaya na kumshushia hadhi yake kwa kumwita Party Crasher na pia mtangazaji mwingine Sherri Shepherd kamwambia anastahili kuwa jela.

Whoopi amedai aliongea maneno ya kawaida ila mume wake aliyekuwa akimpiga picha bila ridhaa yake alimfanya awape maneno ya kuchagua namnukuu “choice words”. Na kwa ujumla alidai alimgusa mama huyu ili ajibu swali alokuwa ameulizwa wakati wa mahojiano na si kumchokoza.

Kazi ipo hizi Reality show zinapendwa mno na baadhi ya watu sababu wanataka kujua maisha ya watu wengine hasa macelebrity kwahiyo nionavyo mimi zitaongezeka kila siku mradi zina watazamaji bila kujali wanajifunza mema au mabaya na alimradi wamiliki wa vyombo vya habari wanatengeneza fedha yao. Kazi iko.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,707 other followers