Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Tiger Woods?

0
467
Tiger Woods
Tiger Woods

Mcheza golf mashuhuri Tiger Woods na mchezaji mwenye kipato cha juu kuliko wachezaji wengine wote duniani amekumbana na kigigingi kingine baada ya kufanya vibaya kuliko mechi nyingine zote tangu aanza kucheza mechi za kulipwa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun  mchezaji huyo yuko chini kabisa hivi sasa baaada ya matokeo hayo mabaya na kumpa nafasi mpinzani wake Jack Nicklaus kuweza kuchukua nafasi ya juu katika mashindano ya mashindao ya Ryder Cup na yale yajayo ya PGA tour.

Tiger woods baada ya kupata kashfa ya ngono amepoteza matangazo kwa asilimia 86 kiasi cha dola milioni 122 kwa mwaka 2010 lakini pamoja na hayo yote bado anakamata nambari moja katika malipo miongoni mwa wanamichezo.

Tiger mwenye umri wa miaka 34 amesema alijitahidi na kuwa mtulivu wakati wa michuano hiyo lakini hiyo haikutosha anategemea kujiandaa zaidi kwa michuano ijayo ya PGA tour akisema anao muda wa kufanya vyema.

Kwa nini bado yupo Nike?

Pamoja na kashfa hizo kampuni kama Nike hazijamwacha Tiger Woods  na hiyo imetajwa kuwa huenda ni kwasababu mwanamichezo huyo ana hisa kwenye kampuni  hiyo na inasemekana Wamarekani wengi hawana tena mapenzi na yeye kama ilivyokuwa zamani.

Wanamchezo wengi na wanasiasa wanaharibiwa maisha na kashfa, ukiangalia yaliomtokea Tiger Woods Novemba mwaka jana juu ya kashfa ya kuwa na wanawake kadhaa nje ya ndoa yake yanaelekea kuwa sasa pengine  ndio yanamharibia Tiger uwezo wake wa kucheza.

Iliripotiwa Tiger Woods anatalikiana na mkewe lakini mengi yamesemwa lakini  karatasi za talaka bado hazijaonekana kwenye mahakama yoyote na zinasubiriwa kwa hamu na waandishi wa habari.

Lakini kwa ujumla kinachoendelea nje ya uwanja wa Golf kwa Tiger Woods hivi sasa kina athari mbaya kwake kwa hiyo kwa ujumla anahitaji kufanya kazi kubwa kurudi katika maisha yake ya kawaida kwani bado kuna mushker ambao haujulikani wazi.na imeripotiwa na ESPN kwamba hivi sasa Tiger Woods hana kocha kulikoni?

NO COMMENTS