BABY SHOWER YA HABIBA YAFANA MARYLAND

Posted in Uncategorized on June 4, 2012 by sunday Shomari

Bi.Habiba akiwa na marafiki zake kulia ni Bi.Aminatha.
Rehema kushoto akiwa na Habiba kulia.
Bi.Rehema Sarmett akiwa kwenmye hafla hiyo ya Baby Shower.

Bi.Habiba akiwa na Geraldine katika shughuli ya Baby shower yake.
Bi.Rehema Sarmett,

MISS MARYLAND NANA MERRIWETHER ASHIKA NAFASI YA PILI

Posted in Uncategorized on June 4, 2012 by sunday Shomari

Miss wetu hapa Maryland Nana Merriwether ashika nafasi ya pili katika mchuano wa kumtafuta Miss USA uliofanyika Las Vegas Nevada.

MISS RHODE ISLAND ASHINDA TAJI LA MISS USA 2012

Posted in Uncategorized on June 4, 2012 by sunday Shomari

Huyu ndiye Miss Rhode Island Olivia Culpo aliyeshinda taji la Miss USA 2012 Jumapili katika mchuano uliofanyika huko Las Vegas Nevada.
Olivia ni mwanafunzi wa Boston University mwenye umri wa miaka 20 na kwa ushindi wake ndiye atakaeiwakilisha Marekani kwenye Miss Universe baadaye mwaka huu.

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA NIGERIA NA KUWA WATU 153

Posted in Uncategorized on June 3, 2012 by sunday Shomari

Maafisa wa Nigeria wanasema abiria wote 153 waliokuwa kwenye ndege ya abiria wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuangukia jengo la makazi mjini Lagos. Rais Goodluck Jonathan ametangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya waathirika na kuamuru uchunguzi wa kina wa janga hilo. Maafisa kutoka idara ya anga ya Nigeria wamesema ndege ya Dana Airlines ilikuwa ikisafiri Jumapili kutoka Abuja kwenda Lagos ilipoangukia jengo la ghorofa mbili kwenye eneo la makazi ya watu wengi na kusababisha majengo mengine kuungua. Yaaminika abiria wote 153 kwenye ndege hiyo wamefariki dunia. Haikujulikana mara moja ikiwa kuna mtu yeyote ardhini aliyeuawa. Shirika la ndege la Dana lina ndege nyingi aina ya Boeing MD-83 ambazo husafirisha abiria kwa saa nzima kutoka Abuja kwenda Lagos.

MBUNGE CCM AKAMATWA KWA RUSHWA

Posted in Uncategorized on June 3, 2012 by sunday Shomari

Omary Badwel.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani jana.

Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.Kusoma zaidi bofya Read more »

KITAMBI NOMA: RAIS KIKWETE KATIKA MAZOEZI YA KUTEMBEA ARUSHA

Posted in Uncategorized on June 3, 2012 by sunday Shomari





Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano wake.(PICHA NA IKULU).

MALKIA ASHEHEREKEA “DIAMOND JUBILEE” MIAKA 60 YA UTAWALA

Posted in Uncategorized on June 3, 2012 by sunday Shomari

Malikia alipokuwa kijana.
Malkia na mumewe Prince Phillip.
Malkia katika gari maalum.
Malkia kwa sasa.
Malkia wa Uingereza Elizabeth aliungana na msururu wa boti zaidi ya 1000 kwenye mto Thames jumapili kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 kwenye utawala wake kama Malkia.

Kwa mujibu wa VOA Maelfu kwa maelfu ya watu walikusanyika mtoni katika siku ya mvua na kushangilia ufalme kwa namna ambayo haijawahi kuonekana katika miaka 350. Rangi nyekundu , nyeupe na bluu za alama ya bendera ya Uingereza zilipamba majengo na watu wakati kengele zikipigwa Uingereza nzima.

Malikia akiwa amevalia rangi ya fedha na nyeupe na kofia alitabasamu na kuwapungia mkono makundi ya watu kutoka kwenye gari lake la kifalme akiwa kandoni mwa mume wake Mwana mfalme Phillip mwenye umri wa miaka 90, mrithi wake mwana mfalme Charles na mtoto wake mkubwa Mwana mfalme William, Mke wa William Kate pia alijiunga na familia, huku akiwa amevaa nguo nyekundu ya Alexander McQueen na kofia inayofanana nayo.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 27 other followers